ODMoja kati ya hatua mhimu sana kwa Mkulima ni kujua hasa namna ya kuandaa eneo lake kabla ya kuingia katika hatua uzalishaji, hivyo basi Jafaido tumekusogezea njia salama ili kukuwezesha wewe Mkulima kujipatia mazao yenye tija kwa kukupatia mbinu bora za kuandaa shamba lako ; kwahiyo Unaweza kutumia trecta, jembe la mkono, ng’ombe kutayarisha shamba,
Kwanza; shamba litayarishwe wiki moja kabla ya kupandikiza miche Kwa kutifua ardhi hadi kufikia kiasi cha sentimita 20 au30.
Pili; lainisha udongo na tengeneza matuta ili kuzuia mmomonyoko katika shamba lako
Tatu; weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha ndoo moja hadi mbili, Kwa eneo la mita mraba 10. Mbolea hii iwekwe katika kila shimo. Kiasi kinachotakiwa ni kilo moja au kopo moja la Tanbond kwa kila shimo. Hii ni sawa kuweka na tani 10 hadi 20 kwa hekta. Katika sehemu zenye upungufu wa madini ya fosiforasi mbolea aina ya N.P.K yenye uwiano wa 5:15:5 itumike. Kiasi kinachotakiwa ni kifuniko kimoja cha maji ya uhai chenye gramu 10 kwa kila shimo la
Mara baada ya hapo ndugu mkulima tegemea ustawi mzuri na wenye tija katika mazao yako.
MAANDALIZI YA SHAMBA KILIMO CHA CABBAGE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment