MAANDALIZI BORA YA KILIMO CHA MBOGA MBOGA NA MATUNDA


MAANDALIZI BORA YA ENEO LA KULIMA MBOGA MBOGA NA MATUNDA 
Katika uchaguzi wa eneo kwa ajili ya bustani zingatia yafuatayo:

Mwinuko
Eneo lisiwe kwenye mwinuko mkali kwa sababu sehemu kama hizo zinaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo. Endapo sehemu itakuwa ya mwinuko tengeneza matungazi (terrace) ili kuzuia mmomonyoko.

Udongo
Udongo unaofaa ni wenye rutuba, mboji nyingi na unaopitisha maji kwa kirahisi. Vilevile usiwe na historia ya magonjwa na wadudu waharibifu.

Chanzo cha Maji
Eneo la bustani liwe karibu na maji ya kudumu. Maji yasiwe na chumvi nyingi kwani huathiri ukuaji wa mimea.

Kitalu
Kitalu kisiwekwe mahali palipo na kivuli kingi kwa kuwa husababisha mimea kuwa dhaifu.
Kuzuia Upepo Mkali

Eneo la bustani lipandwe miti mipakani ili kuzuia upepo mkali. Upepo mkali huharibu mimea kwa kuvunja vunja majani na matawi na husafirisha vimelea vya magonjwa na wadudu. Pia hufanya udongo wa juu kukauka haraka na kuleta mmomonyoko.

5 comments: